Let's Chat

JE KOMPYUTA YAKO INAFANYA KAZI TARATIBU(SLOW)?? NJIA 3 ZA KUONGEZA KASI NA UFANISI WA KOMPYUTA YAKO.

Ushawahi jaribu kufungua faili au app yoyote katika laptopu yako na ikachelewa funguka? Leo katika TechTip apa Ubepari pc tutawapa njia tatu za kuongeza kasi na ufanisi wa Laptopu yako. Acha tuchimbe kwa ndani.

  1. Bonyeza “window key” na “R” kisha uandike neno ” MRT” bonyeza “Enter” na uchague “yes” pia uchague “quick scan” baada ya kuscan na kumaliza ianzishe(restart) kompyuta yako.

2.Bonyeza tena “windows key” na “R” kisha uandike “cleanmgr” na utabonyeza”Enter” kisha uchague “clean up system files” na ubonyeze ok halafu uianzishe(restart) PC yako.

3. Utabonyeza “window key” na “R” kama kawaida kisha andika ” %temp%” na utabonyeza “Enter” kisha chagua mafaili yote ya muda mfupi na uyafute na uianzishe kompyuta yako!

ahsante kwa kuwa pamoja nasi tufollow katika mitandao yetu ya kijamii instagram kwa jina la @ubepari_pc .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *